The House of Favourite Newspapers

Mimi Mars Amkana Marioo Kuwa Mpenzi Wake, Ashikilia Msimamo Wake Kuwa ni Marafiki

0
Mimi Mars ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mdogo wake Vanessa Mdee, akiwa katika picha ya pamoja na Marioo.

 

MIMI MARS; ni mrembo mtangazaji, muigizaji na msanii anayekiwasha kunako Bongo Fleva chini ya Lebo ya Mdee Music inayomilikiwa na Vanessa Mdee ambaye anasisitiza kuwa hakuna uhusiano wa kimapenzi kati yake na msanii mwenzake, Marioo.

 

Mimi Mars ambaye ni mdogo wa wa Vanessa ameshikilia msimamo wake kuwa uhusiano wake na Marioo ni wa kirafiki tu.

“Mimi na Marioo hatupo kwenye mahusiano. Tuna mahusiano ya kirafiki ambayo ni mazuri. Nahisi hicho ndicho kinasababisha watu kusema tupo kwenye mahusiano,” anasema Mimi Mars kwenye Kipindi cha Bongo 255 cha Global Radio.

 

Hata hivyo, Mimi Mars hakutupilia mbali uwezekano wa wao kujitosa kwenye mahusiano katika siku za usoni.

 

“Wakati mwingine urafiki huko mbeleni mambo yakikolea yanaweza kuwa mazuri, lakini ikitokea mtajua. Sisi wenyewe ndiyo tutasema, lakini kwa sasa hakuna kitu,” anasema Mimi Mars.

 

Mrembo huyo anasema kuwa tayari yupo kwenye mahusiano mengine na mwanaume ambaye siyo maarufu, lakini ni raia wa Tanzania.

 

Akizungumzia kitendo cha Marioo kuumizwa na ile video iliyomuonesha akiogelea na Diamond Platnumz nyumbani kwake alfajiri nasema kuwa alikuja kufahamu kuhusu ishu hiyo wakati jamaa huyo alipofunguka.

 

“Sidhani kama nilihitaji kumweleza chochote. Sikujua chochote muda huo eti angeumia. Mimi mwenyewe nilikuja kujua juzi alipoweka kwenye Instastori zake. Hakuwahi kuniambia,” anasema Mimi Mars ambaye anafanya mambo ya hatari ndani ya Tamthiliya ya Juakali.

 

Hata hivyo, aliweka wazi kuwa, hakukerwa na hatua ya Marioo kufunguka kuhusu hisia zake kufuatia tukio hilo.

Stori; Khadija Bakari, Dar

BAADA YA PROFESA JAY KUTOKA HOSPITALI, MKE WAKE AFUNGUKA – “YUKO ENEO MAALUMU”

Leave A Reply