The House of Favourite Newspapers

CEO wa Lebo ya Wasafi, Diamond Amfuata Zari Kenya …Soma Hapa Kujua Kilichowapeleka

0
Zari The Boss Lady

 

Diamond Platnumz au Simba wa Tandale; ni staa mkubwa wa muziki barani Afrika akiiwakilisha vyema Tanzania ambaye juzi alitua nchini Kenya; saa chache baada ya baby mama wake, Zari The Boss Lady naye kutua nchini humo.

 

Diamond ambaye ni CEO wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) hakuweka wazi ziara yake nchini Kenya, bali aliweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa Nairobi, Kenya katika Mgahawa wa Cip Lounge.

 

Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumatano asubuhi na kupokelewa na wenyeji wake Kenya.

Diamond ambaye ni CEO wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Akizungumza na waandishi wa habari, Zari alisema kuwa yuko nchini Kenya kwa shughuli za kibiashara na atazindua jumba jipya la kifahari lililojengwa na Kampuni ya Fine Urban Construction and Interiors Ltd.

 

“Niko hapa kuzindua jumba ambalo limesanifiwa na Fine Urban Construction and Interiors na ni moja ya nyumba za dunia hii ambazo usingetarajia katika Afrika Mashariki. Kwa hiyo niko hapa kuzindua kazi zao.

 

“Natakiwa kufanya kazi na mke wa Gavana (Mike Sonko) na tunatakiwa kutembelea nyumba za watoto. Mimi kuja Kenya na kutojishughulisha na hiyo isingekuwa ziara ya Zari. Napenda chakula cha Kenya, huo ni ugali, nyama choma na sukuma wiki,” alisema Zari.

Leave A Reply