The House of Favourite Newspapers

Mimi Mars Amkingia Kifua Vanessa

0

BAADA ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, dada ake msanii wa Bongo Fleva, Vannesa Mdee ‘V Money’ kuwa yupo bize na mapenzi kuliko kufanya kazi, Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii huyo, ameibuka na kumkingia kifua.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Mimi Mars alisema kuwa, kila mtu ana uhuru wa kufanya kile ambacho anajisikia kufanya, na si kumpangia mtu.

 

“Mimi naona tu mitandaoni wakisema kuwa, dada yangu ameacha kufanya kazi yake yupo bize na Rotimi (mpenzi wake) si kweli, kazi anafanya na pia maisha mengine yanatakiwa yaendelee siyo kama muziki anaupa kisogo, hapana. Wamuache afanye ambacho anajisikia kufanya,” alisema Mimi Mars.

 

STORI | Neema Adrian, Risasi

Leave A Reply