The House of Favourite Newspapers

Miquissone, Chama Wapenya CAF

0

NYOTA wawili wa kikosi cha Simba Luis Miquissone na Clatous Chama wamepenya kwenye kikosi bora cha wiki kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Africa (Caf).

 

Wakati Simba ikitinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita, viungo hawa wote walitupia mabao ambapo Chama alifunga mawili na Miquissone moja.

Jina la Miquissone linakuwa ni mara yake ya tatu kutokea kwenye orodha ya kikosi bora cha wiki cha Caf pia bao lake alilowatunga Al Ahly watakaoukutana nao Aprili 9 lilichaguliwa kuwa bao bora la wiki, kwa Chama ni mara yake ya kwanza kutokea kwenye orodha hiyo.

 

Kwa wazawa ambao wanakipiga Simba ni beki Mohamed Hussein, ‘Zimbwe’ aliweza kutokea mara moja.

 

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ameliambia Championi Jumatano kuwa, ni jambo jema kwa wachezaji kuweza kufi kia hatua hiyo na inawaongezea nguvu kupambana.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply