The House of Favourite Newspapers

Mirabaha ya COSOTA, Mt. Cesilia, Alikiba, Rose Muhando Watikisa

0

Serikali ya Tanzania kupitia Chama cha Haki Miliki (COSOTA) imezindua rasmi Tuzo za Wasanii pamoja na ugawaji wa mirabaha kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan ambae alitaka kuanzia December 2021 Wasanii wawe wanalipwa kutokana na kazi zao kutumika kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Radio na TV.

 

Nyimbo za Kwaya zimeonekana kupigwa na kusikilizwa zaidi katika vituo vya radio na luninga nchini na hivyo kuwafanya waimbaji wa nchimbo za injiri kuibuka na kitita zaidi katika mgao wa mrabaha wa kwanza ulianza kutolewa na COSOTA.

 

Kwaya Kuu ya Mtakatifu Cecilia Arusha imeibuka na mkwanja mzito wa Tsh milioni 8.739 ikifuatiwa na Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba aliyepokea Tsh milioni 7.588 kutokana na mauzo ya nyimbo zake mbalimbali.

 

“Jumla ya milioni 312 zimegawanywa kwa Wasanii na Wanufaika 1,123 wa ndani na nje ya nchi karika mgao huu ambao kazi za muziki 5,924 zilitumika hapa nchini na nje ya nchi,” amesema Doreen Sinare, Mtendaji Mkuu COSOTA.

Wengine waliopokea mgao mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa ni Rose Mhando Tsh milioni 5.79.

1. Mt. Cecilia (Arusha) – Tsh milioni 8.739
2. Ally Kiba – Tsh milioni 7.588
3. Rose Muhando – Tsh milioni 5.79
4. Ambwene Yesaya Tsh milion 5.64
5. Nandy – Tsh millioni 2.61
6. Sarafina – Tsh milioni 1.83
7. Maua Sama
8. Christina Shusho -Tsh milioni 4.5
9. Martha Mwaipaja – Tsh milioni 4.2
10. Emmanuel Mgogo – Tsh milioni 5.6
11. Ambwene Mwasongwe – Tsh milioni 3.43.

Leave A Reply