MIEZI MIWILI BAADA YA NDOA…. MISS TZ AFUMANIWA, ALA KICHAPO!

DUNIA ina mambo! Wakati wanawake wengi waki­itamani ndoa ili kujijengea heshima, mambo yamekuwa tofauti kwa mshiriki wa Miss Tanza­nia 2008, Jackline Chuwa ambaye amekwaa skendo ya kudaiwa kufu­maniwa.

 

Imedaiwa kuwa, Chuwa alifumaniwa na mume wake Leonis Ngasa akiwa na mwanaume mwingine (jina halikupa­tikana mara moja) hivi karibuni wakati ndoa yao ikiwa ingali na miezi miwili tu na ushee.

 

NI TABATA DAR

Imedaiwa kuwa, tukio hilo limetokea maeneo ya Tabata Shule jijini Dar am­bapo shuhuda wa tukio hilo, alilitonya Ijumaa Wikienda kwamba baada ya kufumania, mume wa Jack (Ngasa) alijikuta ametupwa nyuma ya nondo Kituo cha Polisi Tabata-Shule kwa tuhuma za kumpa ‘vitasa’ mkewe.

 

“Yani jamaa alipewa mchongo kwamba mkewe yupo na jamaa sehe­mu maeneo ya Tabata-Shule, akafika fasta sasa kwa kuwa jamaa alikuwa na hasira, akaibua varangati la kufa mtu. “Yule mwanaume aliyekuwa na Jack akatoweka hivyo jamaa akabaki na mkewe na kumtembezea kichapo kikali kwelikweli, alimjeruhi sana damu zikawa zinamtoka kichwani,” kilidai chanzo.

 

AMPELEKA HOSPITALI

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya kumshikisha adabu mkewe na kuona amemuuza sana, alimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Ma­dona kumtibia. “Walipofika pale Ngasa akajaribu kupindisha maelezo kuwa mkewe ame­pata ajali ili kuepuka msala na yeye aweze kuondoka akasema amuokota akiwa amepata ajali, mkewe aliposikia kauli hiyo akaja juu na kusema si kweli bali amempiga.

 

ADAIWA KUINGIA MITINI

“Aliposema hivyo, Ngasa alilazimika kutoweka eneo hilo ambapo Jackline naye alimuunganishia kwa kumui­tia mwizi na ndipo alipofukuzwa na watu wa bodaboda kisha wakamtaiti alipokuwa karibu na Kituo cha Polisi Tabata-Shule. Polisi wakatokea, wakamtia ndani Ngasa, wakalichukua na gari alilokuwa nalo mkewe eneo la tukio kisha mwenyewe wakamkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.”

 

IJUMAA LAANZIA POLISI

Ili kujiridhisha, baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilifunga safari mpaka kituoni hapo ili kupata ukweli wa jambo hilo ambapo askari mmoja wa kituo hicho alikiri uwepo wa tukio hilo lakini akaomba hifadhi ya jina kwa kuwa hana mamlaka ya kuzungumza.

 

Wikienda: (Waandishi wanajitambuli­sha) tumepata madai kwamba kuna mtuhumiwa anaitwa Ngasa alikamatwa baada ya kumpiga mkewe Jackline kwenye fumanizi, ni kweli?

Askari: Ni kweli, yupo mahabusu kwa sababu bado tunaendelea kufanya uchunguzi tena hata gari ya mkewe ipo hapo nje ni Toyota Harrier nyeusi (Ijumaa Wikienda likaipiga picha), ila hatuwezi kuwaruhusu muongee naye wala sisi hatuwezi kuwapa details (maelezo) kamili.

 

JACK AKANA KUFUMANIWA

Baada ya kujiridhisha kuwa mume wa Jack yupo nyuma ya nondo, Ijumaa Wikienda lililazimia ‘kumvutia waya’ Jack ili kujua kama yupo Muhimbili anapatiwa matibabu kama ilivyodaiwa ambapo alipokea simu na kudai kwamba hajafumaniwa lakini akasema amepata matatizo.

“Hizo habari ni za uongo sijui hata mmezitoa wapi jamani kwanza mimi wala sipo Dar nipo Arusha na nina matatizo nimepata ajali kwa sasa nipo hospitali napatiwa matibabu sipendi kuchafuliwa na habari za uongo ja­mani,” alisema Jackline.

 

KUHUSU MUMEWE SASA

Alipoulizwa kuhusu taarifa za mumewe kushikiliwa polisi kwa madai ya kumpa kichapo kwenye fumanizi, awali alikataa lakini baada ya kutumiwa picha ya gari lililokamatwa siku ya tukio likiwa kituo cha polisi, alibadili majibu yake ya awali.

 

“Mimi mwenyewe nimesikia tu yupo kituoni lakini sijajua kapatwa na nini, hilo gari ni langu ila mume wangu hajanifumania huo ni uongo, msiamini kila mnachosikia kwa watu jamani, wengine wana lengo la kunichafua tu mi’ sipendi kabisa hayo mambo,” alisema Jackline na kukata simu.

MCHUNGAJI ANENA

Hata hivyo, Ijumaa Wikienda, lilifani­kiwa kuzungumza na mchungaji aliyewafungisha ndoa Jackline na Ngasa Novemba 3, mwaka jana, Nick Shaboka ambaye pia ndiye alikuwa akihangaikia dhamana ya Ngasa ambapo alikiri kutokea kwa tatizo na kuomba habari hiyo isiandikwe gazetini.

 

“Ni kweli nahangaikia hilo suala na hata jana nilikuwa polisi kwa ajili ya kumuwekea dhamana Ngasa ambaye alikamatwa lakini nawaom­ba msiandike chochote kuhusu hili suala kwa sababu ni aibu kubwa ukizingatia huyo Ngasa ni mchunga­ji kwa hiyo naomba msiitoe kabisa hii habari,” alisema mchungaji huyo.

 

TUJIKUMBUSHE

Ndoa ya Jackline na Ngasa ilikuwa ya kifahari kutokana na jinsi wawili hao walivyojipanga huku ikichangi­wa na watu mashuhuri na vigogo wa nchi na kuifanya iwe harusi yenye hadhi.

Miongoni mwa kufuru zilizooneshwa na wawili hao siku ya tukio ni kufungia kwenye hoteli ya kifahari ya Mount Meru, Arusha huku msafara wao wa magari ukiwa umesheheni magari ya bei mbaya.

Stori: Memorise Richard na Shamuma Awadhi, Dar.

Moto Ulivyoteketeza Nyumba Magomeni, Bibi Amwaga Machozi!

Loading...

Toa comment