The House of Favourite Newspapers

MJADALA MOTO: NAPE, GHASIA KUJIUZULU KAMATI BUNGENI, KUNA NINI?

BUNGE limeahirishwa huku Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye akiwa amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira bila kuweka hadharani sababu za kuachia ngazi.

 

Nape anakuwa mwenyekiti wa tano kuachia ngazi kwenye uongozi wa kamati za bunge tangu bunge la 11 lianze baada ya Hawa Ghasia (Mbunge wa Mtwara-Vijijini) na makamu wake, Jitu Soni, Mbunge wa Babati-Vijijini akafanya hivyo katika Kamati ya Bunge ya Bajeti, Agosti 2018, bila kueleza sababu za uamuzi huo.

 

Hii ilikuwa baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara, Dkt. Dalali Kafumu na makamu wake, Vicky Kamata kujiuzulu Machi 2017, pia bila kutoa sababu ya uamuzi wake.

 

Uamuzi wa wenyeviti na makamu wao (jumla wabunge watato), kujiuzulu umekuwa ukiacha maswali yasiyo na majibu. Unadhani nini sababu ya viongozi hawa kuachia ngazi?

TOA MAONI YAKO, USITOE MATUSI!

Comments are closed.