The House of Favourite Newspapers

ISABELA: NILIKUWA NINALALA NA GODZILLA

MSANII wa Bongo Movies na muziki nchini, Isabela Mpanda ameamua kufunguka ya moyoni kuwa ndiye alikuwa mpenzi wa mwisho kwa Rapa Godzilla ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam.

Isabela ambaye ameonyesha kuguswa na msiba wa rafiki yake huyo wa karibu, amekuwa akiposti picha mbalimbali kwenye ukurasa wake wa Instagram ambazo alikuwa pamoja na Zilla na kudai moja ya shati alilokuwa akivaa Zilla hata yeye Isabela amekuwa akilivaa huku akitupia picha.

Isabela ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Luteni Kalama na mfanyabiashara maarufu, jack Pemba kwa nyakati tofauti, Machi 28, mwaka jana, alibahatika kupata mtoto wa kiume ambapo kwa sasa ananyonyesha, lakini kutokana na kauli yake ya kuwa na uhusiano na Zilla, watu wamekuwa wakihoji kuhusu baba wa mtoto wake huyo mdogo.

Comments are closed.