The House of Favourite Newspapers

Mjane alala nje!

0

IMG_2422GLADNESS MALLYA Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Zakia Onesmo mkazi wa Azimio, Tandika, Dar amepata pigo maradufu baada ya ndugu wa marehemu mumewe kumfungia na hivyo kulala nje, mara tu baada ya kifo na mazishi ya mwenzi wake.

Akizungumza kwa uchungu, Zakia alisema mwaka 2014 alikwenda nyumbani kwao Musoma kumhudumia mama yake aliyekuwa mgonjwa, akimuacha mumewe Kasimu Mandai akiwa mzima na alikaa huko hadi alipopata taarifa ya kifo chake Desemba 16, mwaka jana, hali iliyomlazimu kufunga safari kurejea Dar.

IMG_2417Alidai baada ya kufika Dar alikuta mumewe ameshazikwa msiba ukiwekwa nyumbani kwa mke mkubwa huko Mlandizi Kibaha ambapo naye aliungana na ndugu wengine hadi shughuli hiyo ilipomalizika.

“Baada ya msiba kumalizika niliomba ufunguo ili nirudi nyumbani kwetu nilikokuwa nikiishi na mume wangu Tandika, lakini ndugu akiwemo mtoto mkubwa wa mume wangu aitwaye Yusuf walikataa kunipa funguo wakiniambia marehemu hakuacha maagizo ya mlango kufunguliwa hivyo nisubiri arobaini ipite.

“Nilirudi Tandika nikaanza maisha mapya ya kulala hapa nje kwenye mkeka na hiki chandarua nilisaidiwa na majirani, hivyo nilikaa eda hapahapa mpaka nikamaliza, siku ya hitma (arobaini) ilipofika tuliungana kwa pamoja Mlandizi na siku hiyo ndipo kikao kilikaa.

IMG_2413“Kwenye kikao ndipo waliposoma wosia wa marehemu alioacha ambao ulisema mimi na mwanangu Nuru hatutakiwi kukaa kwenye hii nyumba bali ni ya watoto wa mke mkubwa.

“Nilishangaa kwani mwanangu naye ana haki ya kupewa urithi wa baba yake lakini wakasema kwenye wosia imeandikwa kwamba atarithi kwangu, iliniuma sana, basi nikarudi mpaka sasa nimeshamaliza mwezi nalala hapa nje,” alisema Zakia.

Alisema mtoto huyo mkubwa wa marehemu anayefanya kazi Tazara upande wa bandari, amekuwa akienda kuchukua kodi kwa wapangaji, lakini hampi chochote na wala hampi ufunguo wa chumba alichokuwa akiishi na mumewe, kinyume chake alitoa taarifa kwa mjumbe kwamba watamtolea vitu vyake nje Alhamisi iliyopita.

“Jamani naomba Watanzania wenye uelewa wa sheria ili mwanangu apate haki yake kwani ameacha chuo kwa kukosa ada maana alikuwa akilipiwa na baba yake,” alisema mama huyo.

Mwenyekiti wa mtaa huo wa Azimio Kaskazini, Mshehe Issa amethibitisha kutokea tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi.

Leave A Reply