The House of Favourite Newspapers

Mjengo wa Prof. Jay Wapitiwa na Bomoabomoa

0
Nyumba ya Prof. Jay ambayo imepigwa X.

 

Msanii wa muziki, ambaye ni Mbunge wa Mikuni kupitia CHADEMA, Joseph Haule ‘Professa Jay’, yupo matatani kukosa hifadhi baada ya jumba lake la kifahari alilojenga pembezoni mwa Barabara ya Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, kuwa miongoni mwa nyumba ambazo zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.

 
Nyumbani kwa Prof. Jay.

 

Nyumba za kifahari zilizojengwa pembezoni maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya jijini Dar es Salaam zimekumbwa na bomoabomoa kitu ambacho kimeumiza watu wengi sana, kwani wapo ambao hawana makazi na hawaelewi nyumba zao zikibomolewa wataanzia wapii na wataishi wapi.
 
Prof. Jay na mkewe.

Na nyumba ya Mbunge wa Mikumi ni moja ya nyumba ambazo zimewekewa X kuashiria nayo imo miongoni mwa nyumba za kubomolewa.

 

Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.
 
Nyumba yenyewe ni hii.

 

Tayari Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeshaanza kukata umeme kwenye nyumba nyingi hivyo kuwafanya baadhi ya wenye nyumba kubomoa wenyewe kwa hiari na kufungasha mizigo yao.

 

Tazama picha ya nyumba ya kifahari ya mbunge wa Chadema Joseph Haule maarufu kama Profesa jay ambaye hivi karibuni alifunga harusi kubwa na kuweka jiko ndani.

Yaliyojiri Kesi ya Manji Anayodaiwa Kukamatwa na Sare za Jeshi

Leave A Reply