The House of Favourite Newspapers

Mjue Aliyemeza Kijiko Kikabaki Kooni Mwaka Mzima!

MTU mmoja nchini China hivi sasa anapata ahueni baada ya kuondolewa kijiko kikubwa cha kulia chakula kilichokuwa kimekwama kooni kwa mwaka mzima.

Kwa mujibu wa Hospitali ya Xinjiang Meikuang, mwaka  2017, jamaa huyo ajulikanaye kama Zhang akiwa na umri wa kwenye miaka ya 20, alikimeza kijiko hicho ambapo hakikumpa matatizo yoyote makubwa kiasi kwamba aliweza kuendelea na shughuli zake  kwa miezi mingi bila ya kuhisi maumivu.

Kilichomfanya Zhang agundue tatizo hilo ni pale, Oktoba 2018,  alipopigwa ngumi kifuani na kuanza kulalamika akisikia maumivu yasiyo ya kawaida kifuani na akishindwa kupumua vizuri.  Baada ya kwenda hospsitali akiwa amejishika kifuani kwa maumivu, madaktari waligundua alikuwa na kijiko hicho kooni mwake na hivyo kukitoa kikiwa kimezingirwa na ute mwingi wenye kuteleza.

Baada ya kuondolewa kijiko hicho, Zhang alipata nafuu na madaktari wanasema anaendelea vizuri ambapo ataruhusiwa kuondoka hospitalini siku chache zijazo.

Wakati huohuo, Dkt. Xiwu aliyemhudumia Zhang ametoa onyo kwa watu wengine wasiige na kufanya ‘machejo’ hayo kwani wanaweza kupoteza uhai mara moja.

 

Comments are closed.