The House of Favourite Newspapers

MJUE ZAIDI MKE MTARAJIWA WA DIAMOND PLATNUMZ

Jina lake kamili ni Tanasha Donna Barbieri Oketch lakini pia wakati mwingine kwenye mitandao ya kijamii hujiita Zahara Zaire.

 

Amezaliwa na wazazi wa asili mbili, Mkenya na Mwitaliano,  na amekuwa mwanamitindo kwa kipindi kirefu.

 

 

Alizaliwa Uingereza lakini akahamia Kenya alipokuwa na umri wa miaka miwili ambapo alikulia Kenya hadi alipokuwa na miaka 11 alipohamia Ulaya.

 

Huko, alipata fursa ya kushiriki katika shughuli za mitindo ya mavazi na maonyesho mbalimbali.

 

Ameshiriki katika mashindano mbalimbali yakiwemo Miss Africa Belgium lakini alikiambia chombo kimoja cha habari kwamba alitaka kurejea “nyumbani” na kushiriki shindano la Miss World Kenya, ili awakilishe taifa lake la kuzaliwa.

 

Akiwa Ubelgiji, alisomea somo la utalii.

 

Anaweza kuzungumza lugha tano ambazo ni Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kiholanzi na Kihispania.

 

Ingawa jamaa zake wengine wanaishi Kenya, mamake alibakia Ubelgiji, na kwa mujibu wa mtandao wa Tapmagonline, kwa sasa ana umri wa miaka 22.

 

Tanasha pia ni mwigizaji na mwanamuziki na ana kampuni yake ya nywele inayoitwa  ‘For Her Luxury Hair’ ambayo ndiye mwanzilishi wake na ofisa mkuu mtendaji. Ni kampuni ambayo huuza nywele za binadamu.

 

Oketch alikuwa na uhusiano na mwigizaji Mkenya, Nick Mutuma, ambaye jina lake kamili ni Nicholas Munene Mutuma.

 

 

Uhusiano wao ulifikia tamati mwanzoni mwa mwaka 2017, ambapo Oketch alisema kwamba walikuwa watu “wasiopatana na wasiochukuana” na ndiyo maana wakaachana.

 

Oketch, alishirikishwa kama video vixen kwenye video ya wimbo wa Ali Kiba na Christian Bella  wa  “Nagharamia”.

 

Mapema mwaka huu, alipuuzilia mbali tetesi kwamba alikuwa na uhusiano na mwanamuziki Alikiba.

 

“Kiba na mimi wakati mmoja tuliifanyia kazi video moja ya muziki, lakini hatujawahi kuwa na uhusiano,” alliandika kwenye Instagram.

 

 

Kiba baadaye alifunga ndoa na Mkenya Amina Khaleef.

 

Baada ya video za Diamond kupakiwa Instagram, wafuasi wake wamekuwa wakimfuata kwa wingi Bi Oketch na kumuandikia ujumbe mbalimbali katika ukurasa wake ambapo kufikia sasa ana wafuasi zaidi ya 107,000.

 

Kabla ya hapo, Diamond kwa muda huo alikuwa na uhusiano na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto.

 

 

Hii ni baada ya uhusiano wake wa awali na raia wa Uganda Zari Hassan, ambaye ni mama wa watoto wake wawili kufikia kikomo Siku ya Wapendanao Februari mwaka huu.

 

Baada ya kuhusishwa kwa muda na Hamisa, Diamond alijitokeza na kusema kwamba hakuwa na uhusiano na mwanamke yeyote.

 

 

Kuna utata kwa sasa ikizingatiwa kwamba mapema mwezi huu mamake Diamond, Sanura Kassim, alikuwa amethibitisha kwamba mwanawe alikuwa na uhusiano na mwanamke anayekwenda kwa jina la Kim Nana, ambaye jina lake halisi ni Lilian Kessy.

 

 

Kim Nana ni video vixen pia, na mamake Diamond aliashiria kwamba mwanawe huyo amemshawishi mwanamke huyo kubadili hata dini yake kutoka Ukristo hadi Uislamu, wakijiandaa kufunga ndoa.

 

Diamond aliwahi pia kuwa na uhusiano na Miss Tanzania wa mwaka 2006 wema Sepetu.

 

Comments are closed.