The House of Favourite Newspapers

Mkandarasi Apewa Siku Saba Kabla Mkataba Kuvunjwa

0


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ametoa siku saba kwa Kampuni ya Daska Company Ltd, kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Barabara ya Byuna/Nkindwabiye/ Halawa barabara yenye urefu wa 14.9km. Thamani ya mradi/mkataba huo ni Tsh.139.993 mln.Tofauti na hapo mkataba uvunjwe na taratibu zifuatwe kupata kampuni nyingine.

Sina na sijawahi kuwa na subira kwa wakandarasi wababaishaji. Nitoe wito Wakandarasi wote mkae mguu sawa. Nitafuta kazi zote zinazosuasua ili kubaki na wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mikataba wanayosaini”.Amesema Kafulila.

RAIS SAMIA AMWAMBIA POLEPOLE – “TUTAZUNGUMZA KABLA HUJAENDA MALAWI”

Leave A Reply