The House of Favourite Newspapers

Mkapa Awafunda Wanagenzi Kuwa Viongozi Bora Baadae

0
Rais mstaafu Benjamini Mkapa (kulia) akiwa na viongozi wa Jukwaa la taasisi ya wakurugenzi na wamiliki wa kampuni binafsi (CEOrt), pamoja na washiriki wa mafunzo maalum yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuwa wakurugenzi na maofisa watendaji wa baadae (CAP).

 

RAIS mstaafu Benjamini Mkapa ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Afrika na wadau wa sekta ya biashara kutumia vilivyo rasilimaliwatu iliyopo ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa nchi husika.

 

Mkapa ametoa wito huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanagenzi 16 waliopo chini ya Mpango maalumu wa kutoa mafunzo kwa viongozi wajao (CAP) ambao unaratibiwa na Jukwaa la taasisi ya wakurugenzi na wamiliki wa makampuni binafsi Tanzania (CEOrt) kwa kushirikiana na  Chuo cha Strathmore Business School (SBS).

 

CAP ni mpango maalumu wa kutoa mafunzo kwa Watanzania wenye vipaji na uwezo kitaaluma kushika nyadhifa za juu katika makampuni mbalimbali siku zijazo.

 

Alisema hadi sasa Afrika ina watu zaidi ya bilioni 2.3, wakati idadi ya watu Tanzania nayo ikiendelea kuongezeka hadi milioni 50, uwingi huo wa watu unachangia vilevile katika maendeleo kama ilivyo China na India.

Rais mstaafu Benjamini Mkapa (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la taasisi ya wakurugenzi na wamiliki wa kampuni binafsi (CEOrt), Sanjay Rughani (kushoto) wakizungumza katika darasa maalumu la mafunzo kwa wanagenzi wanaoandaliwa kuwa wakurugenzi na maofisa watendaji wa baadae (CAP).

Aidha, Mkapa ambaye alikuwa mgeni mwalikwa katika mdahalo huo, alitoa wito kwa wanagenzi hao kuheshimu na kujinfunza kwa kupitia wakongwe waliowatangulia kazini ili kupata mbinu nzui za kiuongozi.

 

“Kwa mfano mimi Mwalimu Nyerere ndio aliyenitoa na kunikuza kisiasa, nilikuwa najifunza mengi kuhusu uongozi kutokana na mambo aliyokuwa akiyafanya wakati huo.

 

“Lakini ukishachaguliwa kuwa kiongozi unatakiwa kufanya tathmini na kupitia maamuzi yote yaliyowahi kufanywa katika nafasiuliyonayo ili usahihishe makosa yaliyotendeka na hata kuborehs a kile unachoona ni sahihi kwa kampuni na taasisi unayoongoza kiujumla.

 

“Katika uongozi, ni muhimu kutambua watu wanaofaa kufanya kazi nao na hakikisha unawajua kabisa, hii itakusaidia katika kupiga  hatua katika biashara yako. Vilevile uoneshe  uchangamfu katika utekekezaji wa majukumu yako,” alisema.

 

“Mwishowe, inahitajika kutazama tena uamuzi ambao umefanya au uamuzi uliofanywa na wakurugenzi wako kupitia tena kwa usawa na mara kwa mara ili kufanya marekebisho inapohitajika katika utekelezaji au kufanya maboresho pale inapofafanuliwa malengo,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi mtendaji wa CEOrt, Santina Majengo alisema wamemkaribisha Rais Mkapa kutoa darasa kwa wanagenzi hao ili kuwapiga msasa kutokana na uongozi wake kuweka alama ya mageuzi katika mambo mbalimbali ambayo Tanzania inajivunia hadi sasa.

 

Alisema baada ya kukamilisha mpango huo wa miezi 12, washiriki watakuwa wamepata mafunzo mazuri ambayo yatawasaidia kupiga hatua katika taasisi na makampuni wanayoyatumikia.

 

Alisema kuwa CAP inakusudia kujenga watendaji na wakurugenzi  wakuu wa miaka ijayo kwa kuwapatia maarifa na ujuzi stahiki wa kuongoza.

 

“Pamoja na utajiri wao wa maarifa na utaalam, watendaji wakuu wa sasa wanaweza kutoa ujuzi zaidi kwa kukuza kizazi kijacho cha viongozi wa Tanzania,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa CEOrt, Santina Majengo (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo , Sanjay Rughani (katikati) wakimkaribisha Rais mstaafu Benjamin Mkapa kutoa darasa kwa washiriki wa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kuwa wakurugenzi na watendaji wakuu baadae.

Aidha, alisema washiriki wa mafunzo hayo, wanatoka katika taasisi na makampuni mbalimbali baada ya kuteuliwa na viongozi wao.

 

“Tunazingatia wale wenye elimu kuanzia shahada ya kwanza, ya pili na kuendelea. Lakini pia wale wenye nafasi kama wakuu wa vitengo na idara mbalimbali ambao wanakua kiuongozi,” alisema.

 

Mmoja wa washiriki, Mkurugenzi wa Masoko kutoka benki ya Exim, Stanley Kafu alisema mafunzo wanayopata hususani kwa kushirikisha viongozi wastaafu wenye mafanikio kama Mkapa ni jambo zuri linalowajengea chachu ya kukua kiungongozi.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply