The House of Favourite Newspapers

Mkapa Kuwa Msuluhishi wa Mgogoro wa Burundi

0

mkapaRais wa Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ameteuliwa kuwa msuluhishi wa mgogoro unaoendelea kuikumba nchi ya Burundi kwa muda unaokaribia mwaka mmoja tangu April 2015.

Mkapa ameteuliwa kuwa msulıuhishi wa mgogoro wa huo na marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mkutano uliofanyika jana Jumatano, mjini Arusha.

Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa EAC, Dkt. John Pombe Magufuli aliyasema haya katika mkutano huo mjini Arusha na kuongeza kuwa Benjamin Mkapa ameteuliwa ili kumsaidia rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutatua mgogoro wa Burundi.

Leave A Reply