The House of Favourite Newspapers

Mbavu nje zinavyowateka Wabongo

0

drake-rick-rossDrake na Rick Ross

Makala: BONIPHACE NGUMIJE

KIPINDI cha nyuma ilikuwa ni kawaida kuwashuhudia wasanii wa kiume wa muziki duniani kote hasa wanaofanya Hip Hop wakijiachia kifua wazi wakati wakifanya yao stejini.

Japo suala hili linaendelea hadi sasa vinara wa kufanya hivyo baadhi yao walikuwa ni Marehemu 2pac, Nas, P Diddy, The Game pamoja na 50 Cent.

Kibongobongo wapo walioanika mbavu zao jukwaani ambao ni Dudu Baya, Mwana FA, King Crazy Gk, Chid Benz na wengine wengi.

heres-what-students-learn-in-a-college-course-on-kanye-west-and-jay-zs-relationshipJay Z na Kanye West.

Lakini tofauti na hivyo siku za hivi karibuni suala la kujiachia kifua wazi kwenye shoo limeonekana si kitu na badala yake gumzo hilo limeangukia kwenye ‘vichupa’.

Katika Video ya Trampet ya Jason Deluro alifanya hivyo, Rick Ross kwenye video zake kadhaa ikiwemo Hold Me Back, Martin Music na Every Day I’m Hustling alifaya hivyo.

50-Cent150 Cent

Pia Lil Wayne, Chris Brown, Future, Wiz Khalifa na wengine wengi wametokelezea kwenye video zao mbalimbali wakiwa vifua wazi huku michoro ya tatoo waliyojichora ikitawala kifuani, mgongoni, tumboni na kwenye mikono yao.

naytrueboyNay wa Mitego

Kwa upande wa Bongo wapo Nay wa Mitego. Katika video zake nyingi kama Mr. Nay, Akadumba ambapo ameonekana akiuza mbavu na michoro ya tatoo aliyojichora.

DIAMOND-PLATNUMZDiamond Platnumz

Mwingine ni Diamond Platnumz, kwenye video yake ya Wimbo wa Mdogomdogo, Make Me Sing na nyingine nyingi akiwa yuko kifua wazi.

Jux naye yupo kwenye Video ya Uzuri Wako, Harmonize kwenye Aiyola na Bado, MwanaFA, Young D na wengine wengi kutoka Bongo ambao wamekumbwa na upepo wa swaga hizi.

Leave A Reply