The House of Favourite Newspapers

Mkataba Wa Mido Mpya Yanga SC Watua Rwanda

0

YANGA wanachokifanya ni kumalizana fasta na mastaa wao ambao wanawataka kwa ajili ya msimu ujao ili kuepuka masuala ya kugombania wachezaji.

 

Kwa sasa kilichofanyika mabosi hao wa Yanga mapema tu wamemtumia mkataba kiungo wa Rayon Sport ya Rwanda, Ally Niyonzima kwa ajili ya kumwaga wino.

 

Yanga wako mstari wa mbele katika kumuwania kiungo huyo mwenye sifa za kutengeneza mabao na kufunga baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na klabu yake.

 

Habari ambazo Spoti Xtra, imezipata ni kuwa tayari Yanga wameshamtumia kopi ya mkataba Niyonzima kwa ajili ya kuupitia kabla ya kusubiri majibu kutoka kwake.

 

“Kilichofanyika kwa sasa ni kumtumia Niyonzima mkataba wa awali kwa ajili ya kuupitia na kukubaliana juu ya vile ambavyo vimewekwa kwenye mkataba huo.

 

“Baada ya hapo imetolewa muda kwa ajili ya yeye kurejesha majibu ambapo imefanywa hivyo kwa ajili ya kuepuka kuanza kugombea wachezaji wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa,” kilisema chanzo hicho.

 

Kwa upande wa ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alipoulizwa juu ya ishu hiyo hakutaka kuweka wazi zaidi akisema: “Bado dirisha la usajili halijafunguliwa kwa hiyo ni ngumu kuweka bayana ni nani na nani wanasajiliwa, kitu kikubwa tusubiri kuona dirisha likifunguliwa.”

NA SAID ALLY, Dar

Leave A Reply