The House of Favourite Newspapers

Mke afariki dunia, mume ahaha na mapacha watatu

MKAZI wa Kijiji cha Luegu Kata ya Luegu wilayani Namtumbo, Ruvuma, Said Yasini Simba yuko katika wakati mgumu kufuatia mkewe, kufariki dunia wakati wa kujifungua na kumwachia mapacha watatu.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa na gazeti hili, Simba alisema kifo cha mkewe, Mwanahawa Omar kimemwacha katika hali mbaya kutokana na kumwachia watoto hao wanaotegemea uangalizi wa karibu wa mama.

“Baada ya kifo cha mke wangu, siwezi kufanya shughuli yoyote ya kujitafutia kipato zaidi ya kulea watoto hapa nyumbani kwa kuwabembeleza muda wote maana wanalia tu.

“Mbaya zaidi, hawa watoto wanahitaji maziwa kila wakati hali inayonikumbusha kifo cha mke wangu kila mara na kulia,” alisema Simba.

Alisema mkewe alijifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Songea, Ruvuma wiki iliyopita na kupata mapacha hao watatu.

Comments are closed.