The House of Favourite Newspapers

Mke, Mume Wagombea Mtoto Kortini, Bastola Yatumika!

0

BI-SAADA-AKIWA-NA-MTOTO-WAKSaada Joseph na mwanaye.

Stori: Gregory Nyankaira,  UWAZI

MARA: Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wazazi wawili ambao walikuwa ni mume na mke wamejikuta wakigombea mtoto wao mahakamani kila mmoja akitaka kuishi naye baada ya kupeana talaka katika Mahakama ya Mwanzo Kukirango iliyopo wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.

Katika kesi hiyo ya madai ya talaka namba 02/2016, iliyofunguliwa katika mahakama hiyo na Saada Joseph wa Kariango dhidi ya aliyekuwa mumewe Manyinyi Marwa,  mkazi wa Kijiji cha Mikomariro wilayani Bunda, ambapo mahakama ilitoa talaka Februari 17, mwaka huu.

Mahakama pia iliamuru mlalamikiwa Manyinyi amrudishe mtoto wao (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka mitano, aliyekuwa amemtorosha kutoka kwa mama yake Kiabakari na kumpeleka kijijini kwake Mikomariro tangu mwaka 2014.

Mahakama chini ya Hakimu Erick Kimario ilitoa amri Manyinyi kumpeleka mtoto huyo mahakamani hapo ili akabidhiwe kwa mama yake kwa vile kisheria bado ana umri mdogo unaotakiwa aishi na mama yake mzazi.

Hata hivyo, mlalamikiwa alikaidi amri hiyo na kuapa kutompeleka kamwe mtoto huyo mahakamani hapo ili akabidhiwe kwa mama yake ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani Tabora kikazi hali iliyozua taharuki kubwa katika mahakama hiyo na kusababisha kufungwa baada ya mlalamikiwa huyo kukutwa akiwa na bastola yenye risasi tano kizimbani.

Hata hivyo, alidhibitiwa na polisi na kutiwa mbaroni kwa kosa la kupanda kizimbani akiwa na silaha. Alipoulizwa na gazeti hili ni kwa nini mahakama hiyo ilitoa amri  iliyogomewa na mlalamikiwa, Hakimu Kimario alisema kuwa alishatoa amri ya kukamatwa kwa mlalamikiwa huyo na kukabidhi amri hiyo kwa mkuu wa jeshi la polisi wilayani Butiama kwa utekelezaji lakini mkuu huyo amekaa kimya tangu Februari 17, mwaka huu.

Leave A Reply