The House of Favourite Newspapers

Polisi waua majambazi 3 Arusha

0

bunduki

WATU watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wakiwa na bunduki aina ya AK 47 na milipuko, wameuawa na polisi eneo la Engosheraton-Sinoni mkoani Arusha huku mwanamke akishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alimtaja mmoja wa watu waliouawa kuwa ni Athumani Ramadhani (26) au kwa jina lingine Kassimu na mkewe, Nasri ndiye anashikiliwa.

Alisema wengine hawajafahamika na miili yao iko chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mount Meru ya Mkoa wa Arusha kwa ajili ya uchunguzi na kutoa nafasi kwa wananchi kuwatambua.

Kamanda Sabas alisema Jumamosi iliyopita, asubuhi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba huko Engosheraton–Sinoni, kuna kijana mmoja wanayemtilia shaka kuwa anajihusisha na matukio ya uhalifu.

Alisema waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Athumani na baada ya kumpekua, alikutwa na milipuko aina ya Explogil TMV6 water explosive 17 na Giogel Kubela 10.

Vitu vingine walivyomkuta navyo ni makoti makubwa mawili na kofia moja ya kuficha uso.

Alisema baada ya mahojiano naye, aliwaeleza kuwapo wenzake wawili anaoshirikiana nao katika matukio ya uhalifu.

Leave A Reply