The House of Favourite Newspapers

Mke, mume wazua timbwili studio za radio

0

DSC_5019Wakiwa studio.

Stori:  Dustan Shekidele, Wikienda

Morogoro: Kioja! Mwanamke Betina Kimbe (25) na mumewe, Emmanuel Peter (30), wamezua timbwili ‘hevi’ ndani ya Studio za Radio Planet FM ya mjini hapa baada ya mke kukimbilia redioni akiomba achangiwe nauli ya kurudi kwao mkoani lringa akitaka kumtoroka muwewe kwa sababu alimweka ‘bondi’ wakati wa Mechi ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jijini Dar wiki iliyopita.
Betina alitinga na mwanaye wa mwaka mmoja ndani ya studio hizo akitokea nyumbani kwa baba mtoto wake huko Dumila kwa madai ya kuchoshwa na mumewe huyo huku akimshushia tuhuma lukuki.

MKE ‘AMTUMBUA JIPU’ MUMEWE
Akihojiwa na Mtangazaji Warda Makongwa wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM, Betina alisema aliamua ‘kumtumbua jipu’ mumewe huyo kufuatia mateso aliyokuwa akiyapata kila kukicha.
“Nilipojifungua mtoto huyu, mume wangu alishinda klabuni, aliporudi nyumbani alikuja na mwanamke na kulala naye chumbani kwetu huku mimi akinilaza chini.
“Nilipomhoji, aliniambia ninalea hivyo niwe mpole. Nilikwenda kumshtaki kwa wakubwa, akakanywa.

DSC_5009ADAI KUWEKWA ‘BONDI’
“Wiki iliyopita Simba ilipocheza na Mbeya City aliniweka bondi kwa wanaume wawili akisema kuwa kama Simba ingefungwa walale mimi lakini bahati nzuri Simba ilishinda (mabao 3-0) la sivyo ningekiona cha mtema kuni,” alidai Betina.
Akifafanua tukio hilo lililomfanya amkimbie mumewe, Betina alidai kuwa mbali na ishu hiyo, jamaa huyo alimpeleka kwa mganga wa kienyeji kwa lengo la kumtoa kafara ili apate utajiri lakini alifanikiwa kutoroka.
Mwandishi wetu aliyeshiriki mahojiano hayo alikubaliana na Warda kuiweka hewani namba ya simu ya Betina ili apate msaada huku Warda akitangulia kuchangia shilingi elfu hamsini na mwandishi wetu akatoa elfu ishirini ambapo ndani muda mfupi alichangiwa shilingi laki moja na nusu.

DSC_5029…..Wakielekea polisi.

MUME WA BETINA AIBUKA STUDIO
Katika hali ya kushangaza, zikiwa zimebaki dakika 10 kipindi kifike tamati, mume wa Betina aliibuka studio na kuomba kuingia chumba cha kuendea hewani ambapo aliporuhusiwa alimvaa mkewe huyo ambaye alipomuona alishtuka hivyo kuibua timbwili bila kujali kama walikuwa laivu hewani.
Hata hivyo, katika malumbano yao studio huku wakiwa hewani, Betina alimkana jamaa huyo kuwa siyo mumewe.

MUME ‘ASEVIWA’ BABY
Jamaa huyo alisisitiza kuwa Betina ni mkewe huku akitoa vielelezo ikiwemo namba ya simu ambayo ilipopigwa iliita kwenye simu ya Betina ikionesha kuwa ‘aliseviwa’ Baby.
Baada ya kujiridhisha kuwa wawili hao ni mke na mume, mwanaume huyo naye alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo alisema: “Huyu mke wangu aliniambia kaka yake anatoka Dar kwenda lringa hivyo aliomba akutane naye Msamvu (Stendi ya Mkoa wa Morogoro), sasa nimeshangaa kumsikia redioni akininanga.”

DSC_5034Watu wakiwa eneo la tukio.

BETINA ALIWEKWA BONDI?
Kuhusu kumuweka mkewe bondi, Emmanuel alisema: “Kweli mimi ni shabiki wa Simba na ule ulikuwa ni utani tu. Kuhusu kwenda kumuua kwa mganga amedanganya.”
Baada ya wasikilizaji kusikia kasheshe hiyo hasa wale waliomchangia Betina, walichukukizwa na tukio hilo hivyo wakaibuka nje ya studio hizo wakitaka warudishiwe fedha yao.
Kwa upande wake, Warda ilibidi atoe taarifa polisi huku akimtuhumu Betina kuwa alitaka kujipatia fedha kwa udanganyifu.

SOO LATINGA POLISI
Kwa sasa msala huo uko Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati mjini hapa huku ndoa ya wawili hao ikiwa kwenye sintofahamu kama wataendelea kuwa pamoja au ndiyo mwisho wao.

Leave A Reply