The House of Favourite Newspapers

Umeelewa Kiasi Gani Kabla Ya Mitihani?

0

Wanafunzi wengi makini hujisomea kwa bidii mara kwa mara kabla ya mitihani yao huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufaulu.

Bahati mbaya huja pale wanafunzi hao watakapojikuta wanafeli sawasawa na wanafunzi wengine ambao walikuwa hawajibidiishi kwenye masomo yao.

Baadhi yao huendelea kujisomea zaidi na zaidi wakiamini kwamba kufeli kwao kumetokana na juhudi ndogo walizozifanya katika kujisomea, lakini ukweli ni kwamba wanafunzi wengi mara baada ya kujisomea hawajiulizi wameelewa kiasi gani kabla ya kuingia kufanya mitihani yao.

Kabla ya kuingia hatua hii muhimu wanafunzi hutakiwa kuwa tayari kiakili na kujiamini kwa asilimia nyingi kuwa hakika wameelewa masomo yao ipasavyo kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani.
Mambo muhimu ambayo mwanafunzi hupaswa kujipima nayo ni:-

MITIHANI YA ZAMANI (PAST PAPERS)
Mitihani hii huwa na faida kama vile, Kumpima mwanafunzi kama anajua jinsi maswali yanavyoulizwa; Kujua idadi ya maswali yanayotoka kwa ‘topic’ tofauti, wingi wa ‘maksi’ kwa kila swali, hii pia humsaidia mwanafunzi kujua kasi yake katika kuyajibu maswali yake.
Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply