The House of Favourite Newspapers

Mke wa Deo Filikunjombe, Waziri Mambo Hadharani

Deo Haule Filikunjombe enzi za uhai wake akiwa na mkewe, Sarah Habiba.

Mambo ni moto! Ubuyu ulionyooka uliolifikia gazeti hili unadai kuwa, waziri mmoja mchapakazi (jina tunalihifadhi kwa sasa), anadaiwa kurithi mikoba ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa mkoani Njombe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Deo Haule Filikunjombe kwa ‘kujiweka’ kwa mkewe, Sarah Habiba, Ijumaa lina habari kamili.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Awali, vyanzo vilivyo karibu na Sarah, vilishusha madai kuwa, waziri huyo kijana, amekuwa akitinga nyumbani kwa marehemu anapoishi Sarah na watoto wake watatu wa kiume, Mtoni-Kijichi jijini Dar.

“Yaani tunashangazwa sana na ujio wa huyu waziri. Unajua bora kama ingekuwa ni mtu wa mbali, lakini huyu alikuwa karibu sana na marehemu Deo na anamfahamu vizuri, iweje leo aje amrithi rafiki yake?

“Si mara moja au mara mbili, tunamuona mara kwa mara anakuja hapa nyumbani. Akija anakaa weee…baadaye ndo’ anaondoka. “Unajua hii haileti picha nzuri. Bora hata angekuwa mtu wa mbali, lakini si huyu ambaye alikuwa akimfahamu vizuri marehemu. Hii inaleta picha kwamba huenda alikuwa akimtamani mke wa mwenzake hata kabla Deo hajafariki dunia,” Chanzo kilishusha madai hayo mazito.

 

MADAI ZAIDI

Chanzo hicho kilizidi kushusha madai kwamba, waziri huyo ndiye ambaye anampa kampani Sarah hata kwenye mambo mbalimbali ya kifamilia hivyo kuashiria kuwa wawili hao ni ‘damdam’.

“Waziri ana mawe, nasikia ndiye anayesimamia mpango mzima hadi mambo ya shule ya watoto pamoja na vurugu za Sarah, mheshimiwa anakata mkwanja,” kilidai chanzo hicho.

 

MKE WA DEO AANIKA UKWELI

Baada ya kupata madai hayo, Ijumaa lilimtafuta mke wa Deo na kumwekea mezani madai hayo yote ambapo aliyakanusha vilivyo na kusema anayashangaa yametokea wapi.

“Siyo kweli. Nasema siyo kweli, hivyo vitu ninashindwa kuelewa hata vinatokea wapi? Wanaleta hayo maneno bila kuwa hata na ushahidi wala ukweli wowote.

“Sasa hebu angalia wanasema kuhusu watoto wewe mwenyewe (anataja jina la mwandishi) unajua, watoto ninawasomesha mwenyewe. Namshukuru Mungu najimudu kuwasomesha wanangu na kufuatilia maendeleo yao kimasomo,” alisema Sarah.

 

ANAPAMBANA MWENYEWE

Kama hiyo haitoshi, Sarah alifafanua kuwa, anapambana mwenyewe kwenye maisha yake na anamshukuru Mungu anapata fedha zake halali za kusukuma maisha.

“Nina mashamba yangu, ninajituma kwa jasho langu halafu mtu anaamka tu na kuropoka mambo ya uongo tu. Kwanza wanaweza hata kunisababishia nisizungumze na watu hata wakanisaidia kwa ajili ya mambo yao ya uongo,” anazidi kuongea mama Deo huku akionesha wazi kukerwa na madai hayo aliyoyaita hayana mashiko.

 

AKIRI WAZIRI KUFIKA KWAKE

Alipoulizwa kuhusu waziri huyo kufika nyumbani kwake, alikiri kuwa ni kweli anafika kama wanavyofika waheshimiwa wengine ambao walikuwa marafiki wa marehemu mumewe.

“Kweli huyo waziri alikuja, tena sijui mara mbili hivi na si yeye tu, wanakuja mawaziri wengi tu waliokuwa karibu na marehemu mume wangu na familia kwa jumla.

“Watu wanakuja kuangalia familia nitawakataza? Mtu kuja nyumbani tu ni tatizo? Mbona hawawasemi wabunge kama Zitto na Kangi ambao wanakuja mara kwa mara kunisalimia?

“Huu ni ujinga. Wamuache waziri wa watu afanye kazi, wasimharibie mambo yake na familia yake kwa kuzusha maneno yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

 

“Mimi kweli bado ni kijana, lakini ninamshukuru Mungu ninajitambua. Siwezi kufanya mambo ya kijinga kama hayo. Naanzaje kutembea na rafiki wa mume wangu? Waniache jamani nipumzike,” alisema Sarah.

Sarah alisema kuwa, anamuomba Mungu azidi kumbariki kwani anaamini maneno kama hayo yanazushwa na watu wasiopenda kumuona mwenye furaha, lakini kwa uwezo wake Mungu, hawataweza.

“Ninajituma sana, napigania furaha yangu kwa namna yoyote na sipo tayari kuona inapotea. Mungu atanipigania, wataibua uongo wao, lakini mwisho wa siku watabaki na aibu maana hakuna uongo unaoweza kuushinda ukweli,” alisema mama Deo.

 

WAZIRI ANASEMAJE?

Jitihada za kumpata Waziri anayetajwa zilifanyika kwa kumpigia simu kupitia simu yake ya mkononi lakini kila ilipopigwa haikupokelewa.

Alipotumiwa ujumbe wa maneno (unaoonekana ukurasa wa mbele) hakujibu mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni.

 

TUJIKUMBUSHE

Marehemu Deo Haule Filikunjombe alifariki dunia Oktoba 15, mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, katika ajali ya chopa iliyokuwa na usajili namba 5Y-DKK ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Selous ambapo watu wengine watatu walifariki dunia akiwemo rubani William Silaa, aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Egdi Mkwera na aliyekuwa Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Vitalis Blanko Haule.

 

Imeandikwa na Erick Evarist, Brighton Masalu na Gladnes Mallya.

STORI: WAANDISHI WETU, IJUMAA | DAR ES SALAAM

Comments are closed.