The House of Favourite Newspapers

Mke wa El Chapo Ahukumiwa Jela

0

Emma Coronel Aispuro amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

 

Emma ni mke wa mlanguzi maarufu wa madawa ya kulevya nchini Mexico aliyeko gerezani Joaquin “El Chapo” Guzman.

 

Adhabu hiyo ilikuwa chini ya ile ya miaka minne iliyoombwa na waendesha mashitaka, huku jaji aliyetoa hukumu hiyo akikiri kuwa Coronel alikuwa bado kijana mdogo wakati alipoolewa na mlanguzi huyo hatari wa dawa za kulevya na tayari alikuwa amekiri kuwa na hatia baada ya kukamatwa mnamo Februari 2021.

 

Coronel mwenye umri wa miaka 32 aliomba radhi mahakamani akisema anajutia madhara yoyote aliyosababisha na kumuomba Jaji kumuwezesha kuwalea mabinti zake mapacha wenye umri wa miaka tisa.

Leave A Reply