The House of Favourite Newspapers

Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama Haikumkuta na hatia – Video

0


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewaachia huru, Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Bilionea Erasto Msuya, pamoja na mwenzake Revocatus Everest, waliokuwa wakikabiliwa na shtaka kumuua kwa kukusudia Aneth Elisaria Msuya, ambaye ni wifi yake Mariam, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kama watuhumiwa walifanya kosa hilo.

Akisoma Shitaka hilo Jaji wa Mahakama Kuu, Edwin Kakolaki amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kama watuhumiwa walifanya kosa hilo, huku akiongeza kuwa ushahidi wa kimamzingira unaonyesha kuwa wahuska kwa namna moja ama nyingine walihuska katika mauaji hayo, japo hakuna ushahidi wa kutosha kuwa kweli ni wao walifanya tukio hilo, moja kwa moja au la.
Mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Steven Mrita na Mshtakiwa Mwenzake Bw.Revocatus Everest, Mahakamani

Jaji Kakolaki amesema, Mshtakiwa wa pili, ambaye ni Bw.Revocatus Everest, vinasaba vilivyochukuliwa katika eneo la tukio kupitia kisu, filimbi na chupi vinaonyesha kuwa, alikuwa navyo au alisaidia kufika eneo la tukio, ambapo amebainisha kuwa licha ya vinasaba kuonyesha hivyo, lakini mahakama imeshindwa kuthibitisha kama ndivyo vilivyotumika katika tukio hilo kutokana na kutokuwepo kwa vinasaba vya Marehemu Aneth.

Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, Miriam na mwenzake Muyella wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth, Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Aneth alikuwa mdogo wa bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SMG, katika eneo la Mijohoroni, Barabara Kuu ya Moshi-Arusha wilayani Hai,mkoani Kilimanjaro, Agosti 7, 2013.

Leave A Reply