Mke wa Masele Ashauriwa Ajiande kwa Vicheko Kibao

masele-chapombe-1

Masele na mkewe, muda mfupi baada ya kufunga ndoa.

BI Specioza Malick  Mke wa msanii wa vichekesho nchini aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa kuchekesha, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’,  ni vyema akajitayarisha kucheka na kuvunjika mbavu kutokana na sanaa hiyo ambayo mumewe anaiweza ilivyo.

masele-chapombe-3

Mrembo huyo, aliyefunga ndoa na msanii huyo mwezi huu wa Januari,  ameshauriwa na mashabiki wa sanaa ya mumewe ajitayarishe kucheka zaidi na wakati huohuo awe na ubavu wa kutenganisha kazi ya Masele na maisha yake halisi.

masele-chapombe-7

“Mke wa Masele ajiandae kucheka mpaka kuumwa mbavu siku Masele akiamua kumletea nyumbani vituo anavyofanya kwenye televisheni nyumbani.   Bi Specioza ajiandae kuwa maarufu kwani kwa sasa ameungana mwili mmoja na mtu maarufu nchini,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kama Bondi Masaba wa jijini Dar es Salaam.

Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi-Makabe jijini Dar es Salaam.

Na Salum Milongo/GPL

Maisha Halisi ya Mshindi wa Nyumba ya Global Publishers


Toa comment