The House of Favourite Newspapers

Mkojani Ataja Siri Ya Filamu Zake Kupendwa Kwenye Mabasi Ya Mikoani

0
Mkojani.

Msanii wa filamu za vichekesho, Abdalah Zunda maarufu kwa jina la Mkojani ambaye filamu zake zimejipatia umaarufu mkubwa kwenye mabasi yaendayo mikoani amesema wenye mabasi hayo ndiyo walioanza kugundua kipaji chake na wakafanya mpaka wengine nao wazoee filamu zake nao kumuelewa.

Akizungumza na Global Tv, Mkojani amesema baada ya kugundua upepo wake uko zaidi kwenye mabasi ndipo sasa amejikita zaidi kutengeneza filamu ambazo zinawafurahisha zaidi abiria ili azidi kujiimarisha kwenye soko hilo.

Mkojani amesema hayo kwenye tamasha la usiku wa Tuzo za Filamu 2023, lililoandaliwa na Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu  lililofanyika Ukumbi wa The Super Dome Masaki, Dar.

Msanii huyo aliyeimwagia sifa Bodi ya Filamu kwa kurejesha heshima ya tasnia ya filamu hapa nchini ameibuka na tuzo mbili kwenye tamasha hilo, Msanii Bora wa Komedi na filamu bora ya komedi akimuangusha Joti ambaye moja ya filamu zake ilishinda kwenye vipengele vya komedi. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GLOBAL PUBLISHERS 

Leave A Reply