The House of Favourite Newspapers

Maskini Latifa! Ana Miaka 17 Amekakamaa, Wakimkunja Anavunjika, Ndugu Wamwita Msukule – Video

0

Ukimtazama kwa haraka huwezi kuamini macho yako kama kuna binadamu wanateseka kiasi hiki!

Anaitwa Latipha Ibrahim Kadogosa, mwili wake umekakamaa, ukuaji wake ni wa kusuasua, ana umri wa miaka 17 lakini ukimtazama utafikiri bado hajafikisha hata miaka 10!

Latipha anateseka kwa sababu ya uzembe wa madaktari uliofanyika wakati anazaliwa.

Mama yake, Rehema Abdallah Kadogosa anasimulia madhila anayoyapata kutokana na hali ya mwanaye huku baba wa mtoto akimtelekeza kwa sababu ya ulemavu wa mwanaye.

Mbaya zaidi, baadhi ya majirani wanamtuhumu kuwa eti ni mchawi na amemchukua mwanaye msukule! Inahuzunisha.

Mtoto Latipha anahitaji msaada wako wewe utakayeguswa. Unaweza kuwasiliana na mama yake, Rehema kwa simu 0762 075 573, jina Rehema Kadogosa.

Leave A Reply