The House of Favourite Newspapers

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge la Kumi na Mbili Kuanza leo Dodoma

0

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge la Kumi na Mbili umepangwa kufanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia leo tarehe 30 Januari hadi tarehe 16 Februari, 2024.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Ofisi ya Bunge imebainisha kuwa Mkutano huo umeongezewa wiki moja kutokana uzito wa majukumu yaliyopangwa ikiwemo uzito wa Miswada itakayoshughulikiwa.

Miswada ambayo imepangwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.

Miswada mingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023.

Vilevile katika Mkutano huu wa Bunge Kamati za Kudumu za Bunge zitawasilisha taarifa za shughuli zilizotekelezwa na Kamati kwa mwaka 2023.

Aidha, wastani wa Maswali 250 ya kawaida na Maswali 24 ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge.

Leave A Reply