The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na taasisi ya Lalji Foundation , wametoa msaada wa Sh milioni 10 kwa wafanyabiashara 50

0

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akishirikiana na taasisi ya Lalji Foundation , wametoa msaada wa Sh milioni 10 kwaajili ya mitaji kwa wafanyabiashara wadogo 50 kutoka kata ya Kivukoni.

Mkuu wa mkoa, Albert Chalamila akiwa na Larji Foundation

 

katika Msaada huo kila mjasiliamali aliweza kukabidhiwa Sh laki 2, kwaajili ya kuinua biashara yake ambapo wengi wao wanajishughulisha na uuzaji wa samaki, chakula na vinywaji.

Akizungumza na Wafanyabiashara wakati akiwakabidhi misaada hiyo jana mkoani Dar es Salaam, Chalamila alisema fedha hizo zikatumike kwaajili ya kuinua mitaji yao na kujiinua kiuchumi.

Alisema anatamani kuona wajasiliamali hao, wakiziangalia fedha hizo sio kwa ukubwa ila zitakavyoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi baada ya mwaka mmmoja baada ya kukabidhi kwa kukuza biashara zao.

“Tunajua mnashida ya mitaji na mmekuwa mkikopa fedha za mikopo umiza kutoka katika taasisi za kifedha na kujikuta mkilipa kila siku na wengine kushindwa.

Msiwe mnakopa kila taasisi ya kifedha inayokuja kwako, muwe mnakopa kwa stara na isiyoumiza” alisema Chalamila.

Aliongezea kwa kusema wapo watu ambao wamekuwa wakichukua mikopo kwa lengo la kujiendeleza biashara kutoka katika taasisi za kifedha na baadaye inapowashinda wanaoenda ofisini kwake kuomba Msaada.

Wakati huo huo mkurugenzi wa Lalji Foundation,Imtiaz Lalji, alisema walitembelea katika soko la kivukoni

Alisema lengo Lao ni kuwasaidia ili waweze kukidhi mahitaji yao, waweze kujiendeleza kiuchumi ili iwasaidie katika maisha yao.

“Ni taasisi ya kifamilia ambayo tumezaliwa hapa nchini, lakini wengine wapo nchi zingine na kwa pamoja tumeona kile tunachokipata kusaidia wengine.

Tayari tumeshasaidia watu wenye matatizo ya macho 348 katika Hospitali ya Kahama, lakini pia tulishatoa futari kwa watu 200 katika mwezi mtukufu wa ramadhani” alisema Lalji.

Kwaniaba ya wajasiliamali waliopata mtaji huo, Rahilu Nyundo alishukuru kwa kupata mitaji hiyo na kusema itawasaidia katika kukuza mitaji yao.

Alimalizia kwa kusema wanaweza kutembelea biashara hizo ili kuona hali ilivyo kwa sasa na wanapoelekea .

Leave A Reply