The House of Favourite Newspapers

Mkwasa ashitakiwa Fifa

0

CharlesBonifaceMkwasa1 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa.

Na Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Wanasoka wa Algeria, Ahmed Boudry ameamua kumfungulia mashitaka Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa.

Boudry amesema wamekerwa kupita kiasi na kauli ya Mkwasa kwamba raia wa Algeria ni wabaguzi wakubwa wa rangi, hivyo amemfungulia mashitaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

“Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hata kabla ya mechi ambayo Tanzania ilifungwa bao saba. Tunaamua kumfikisha Fifa kwa kuwa amewadhalilisha raia wote wa Algeria wakiwemo wachezaji.

“Hakuwa na ushahidi, Tanzania imekuja hapa zaidi ya mara moja na hatujawahi kupata malalamiko ya ubaguzi wa rangi, vipi yeye Mkwasa aseme hayo?” alihoji kiongozi huyo.

Kabla ya kauli yake hiyo, vyombo vingi vya habari vya Algeria vilizungumzia suala la Mkwasa kusema Waalgeria ni wabaguzi wa rangi. Vyombo hivyo vya habari vya Algeria ikiwemo mitandao inayotumia lugha ya Kifaransa vilimshambuliaji Mkwasa kwa madai amewakashifu Waalgeria.

Algeria iliing’oa Stars kwa kuifunga mabao 7-0 katika mechi ya marudiano mjini Blida ambayo ilikuwa ya kufuzu Kombe la Dunia 2018. Stars imeaga michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya mabao 9-2 kwani awali ilitoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa.

Leave A Reply