The House of Favourite Newspapers

Mlela ageukia Bongo Fleva

0

Msanii Yusuph Mlela 'Angelo'

Staa wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela.

Suzan kayogela
BAADA ya kuegemea upande wa filamu kwa muda mrefu, hatimaye staa wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela ameamua kugeukia Muziki wa Bongo Fleva rasmi ili kutimiza ndoto zake za muda mrefu alizokuwa nazo.

Akistorisha na kona ya Bongo Muvi Mlela alisema kuwa, kabla ya kujikita kwenye uigizaji alikuwa na nia ya kuanza kufanya muziki lakini baadaye alikuja kubadili uamuzi na kufanya filamu ambazo zimemletea heshima kubwa.

“Nimeshatengeneza ngoma yangu ambayo ipo mbioni kutoka inayokwenda kwa jina la Mrembo, mashabiki wakae tayari kuipokea,” alisema Mlela.

Leave A Reply