The House of Favourite Newspapers

Mlinzi wa Malkia Elizabeth II Aanguka Ghafla Kwenye Ukumbi wa Westminster Hall

0

Mlinzi wa Malkia Elizabeth II leo Septemba 15, ameanguka ghafla wakati maandalizi ya kuagwa kwa mwili wa Malkia kwenye ukumbi wa Westminster Hall jijini London chanzo cha kuanguka kwa mlinzi huyo haijafahamika mara moja.

 

Baada ya kuanguka kwa mlinzi huyo matangazo ya Televisheni ambayo yalikuwa ‘Live’ yalisitishwa kwa muda wakati mlizi huyo akipatiwa huduma ya kwanza.

 

Tukio hilo limetokea wakati raia wa Uingereza wakiendelee na zoezi la kuaga mwili wa Malkia aliyefariki siku ya Alhamisi huko Balmoral, Scotalnd.

 

Jeneza la Malkia linalindwa kikosi maalum kinachofahamika kama Sovereign’s Bodyguard.

Malkia Elizabeth II atazikwa Septemba 19 ambapo wakuu mbalimbali wa mataifa wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.

Leave A Reply