The House of Favourite Newspapers

Mlipili atoweka Simba

BAADA ya kusugua benchi kwa muda mrefu msimu huu bila ya kupata nafasi ya kucheza wala kukaa benchi, beki wa kati wa Simba, Yusuf Mlipili, ameamua kujiondoa katika kikosi cha timu hiyo.

Mlipili ambaye alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea Toto Africans ya jijini Mwanza, anadaiwa kutimka zake katika kikosi cha timu hiyo yapata wiki sasa.

 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa Mlipili amefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa hana nafasi katika kikosi cha timu hiyo msimu huu, tofauti na msimu uliopita ambapo alikuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

 

“Kwa hiyo hata viongozi hawajui alipo kwa sababu kaondoka bila ya kutoa taarifa na sasa yapata wiki, mazoezi yote tuliyofanya ya kujiandaa dhidi ya Alliance FC pamoja na Ruvu Shooting haku­wepo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems kuhusiana na mchezaji huyo alise­ma kuwa hana taarifa zake zozote hivyo hawezi kumzungumzia.

 

“Sina taarifa zake kwa hiyo si­wezi kusema chochote kuhusiana naye,” alisema Aussems.

Hata hivyo, alipotafutwa Mlipili ili aweze kuzungumzia hilo, hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

LIVE: KUAGWA KWA ISACK GAMBA, MAJONZI & VILIO VYATAWALA

Comments are closed.