The House of Favourite Newspapers

Mmarekani Mwingine Mweusi Auawa na Polisi

0

MTU mmoja mweusi nchini Marekani, Daniel Prude, amefariki dunia baada ya kundi la polisi nchini humo kumvalisha kofia na kisha kugandamizwa kichwa chake kwenye barabara ya lami kwa dakika mbili.

 

Inaaminika kuwa, Prude aliuawa Machi 3, 2020, baada ya kufanyiwa tukio hilo kisha watoa msaada wa huduma za afya kumwahisha hospitali na kupoteza maisha siku saba baada ya kufanyiwa tukio hilo.

 

Kifo chake hakikufahamika na watu wengi kabla ya jana familia yake kufanya mkutano na waandishi wa habari kisha kuachia kipande cha video kikiwaonyesha polisi walivyomfanyia tukio hilo.

 

Kaka wa Prude, Joe, alihoji, “Ni wangapi watapoteza maisha katika jamii mpaka watu waelewe kwamba haya matukio yanapaswa kupigwa vita?”

Leave A Reply