The House of Favourite Newspapers

Mnigeria Ateuliwa Katika Bodi ya Washauri wa Uchumi wa Donald Trump

bayo-ogunlesi
RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mfanyabiashara raia wa Nigeria, Adebayo Ogunlesi (pichani juu), kuwa mmojawapo katika bodi ya washauri wake wa masuala ya uchumi.

Tovuti ya Business Insider imeeleza kuwa bodi hiyo aliyoiteua imejaa mabilionea akiwemo Ogunlesi ambaye ndiye Mwafrika pekee.

Ogunlesi aliyezaliwa katika Jimbo la Ondo nchini Nigeria ni mhitimu katika vyuo vya Oxford na Harvard, pia ni Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa makammpuni ya Global Infrastructure Partners.

Baba mzazi wa Ogulesi ndiye alikuwa profesa wa kwanza wa udaktari nchini Nigeria.

a-deal-for-donald-trump-b

Wajumbe wengine aliowateua Trump katika bodi hiyo ni pamoja na;

Mwenyekiti wa Bodi, Stephen Schwarzman ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Blackstone.

Paul Atkins, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa General Motors
Toby Cosgrove, Mkurugenzi Mtendaji wa Cleveland Clinic
Jamie Dimon, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa JPMorgan Chase & Co.
Larry Fink, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa BlackRock
Bob Iger, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa The Walt Disney Company
Rich Lesser, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Boston Consulting Group
Doug McMillon, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Wal-Mart Stores Inc.

Jim McNerney, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Boeing
Ginni Rometty, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa IBM

Kevin Warsh, Mjumbe wa zamani wa Bodi ya Magavana wa Federal Reserve System
Mark Weinberger, Mwenyekiti wa dunia na Mkurugenzi Mtendaji wa EY
Jack Welch, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa General Electric
Daniel Yergin, Mshindi wa Tuzo ya Pulitzer na Makamu Mwenyekiti wa IHS Markit

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kundi hilo litamshauri Trump jinsi ya kuweka mipango itakayochochea ukuaji wa upatikanaji ajira na kuongeza uzalishaji nchini Marekani

Comments are closed.