The House of Favourite Newspapers

Mo aikwepa Simba Taifa

WAKATI mashabiki wa Simba, wakitarajia kumuona mwekezaji wao, Mohamed Dewji ‘Mo’ uwanjani jana, mambo yalikuwa tofauti kwani kigogo huyo hakutokea.

 

Taarifa zilizagaa kwa kasi juzi na kusambazwa kwenye vituo mbalim­bali vya redio kwamba Mo angehud­huria mechi ya jana kati ya Simba na Stand United, na mashabiki walikaa mkao wa kumsubiri.

 

Hiyo ilikuwa ni siku chache baada ya bilionea huyo kijana kupatikana, kufuatia kutekwa na watu wasiojulikana na ku­fichwa kwa zaidi ya siku tisa tangu Alhamisi ya Oktoba 11 hadi alipopa­tikana juzi Ijumaa usiku.

 

Ilielezwa kuwa Mo angeibuka uwanjani jana kwa ajili ya kuwasalimia Wanasimba na kuwashukuru kwa kumuombea alipokuwa matatizoni. Hata hivyo, pamoja na kutoonekana kwake uwanjani, Simba ilishinda 3-0.

Comments are closed.