The House of Favourite Newspapers

MO Dewji: Kijana Akifanya Haya Atatengeneza Mkwanja Kirahisi

Mo Dewji.

MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group amefunguka na kuwapa siri vijana wa Tanzania kuwa wanapaswa kujikita zaidi katika kilimo kwani ndipo sehemu ambayo ina pesa nyingi sana.

Dewji alisema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya kituo cha habari na kusema kuwa yeye anatengeneza fedha nyingi zaidi kupitia kilimo ambacho anakifanya na kwamba anatengeneza faidi kubwa kupitia kilimo cha chai, korosho na katani. 

 

“Niwambie siri moja vijana wenzangu kuna pesa nyingi sana kwenye kilimo, mimi nipo kwenye kilimo nipo kwenye katani, nipo kwenye chai, nipo kwenye korosho na ninatengeneza fedha nyingi sana kupitia kilimo” alisisitiza Mo Dewji.

 

Mbali na Mohammed Dewji watu wengine maarufu ambao wamejikita kwenye kilimo ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu wa awamu ya nne Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

Mzee Makamba Atema Nyongo CCM, Awapa Makavu Lowassa na Mbowe

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Comments are closed.