The House of Favourite Newspapers

Mo Dewji: Ninawashukuru, Mungu Awazidishie kwa Wema Wenu

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohammed Dewji amemshukuru Mungu kwa kumrejesha salama kutoka kwenye mikono ya watekaji huku akiwashukuru Watanzania kwa kumuombea na kumwepusha na mabaya katika kipindi cha siku 9 alipokuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

Mo ambaye alitekwa alfajiri ya Oktoba 11 na kuachiwa usiku wa Oktoba 20, amerejea mtandaoni kwa mara kwanza na kuandika;

 

“Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima,” Mo aliandika.

LEMA “Wamenihoji kisa Mo Dewji, LUGOLA nitamnyoosha, Siogopi”

Comments are closed.