The House of Favourite Newspapers

TIGO PESA KULIPA MPAKA MILLION 10 KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imeongeza kiasi cha kulipa wakulima wa korosho kutoka shilingi Million tatu na sasa wataweza kulipwa shilingi million kumi za malipo ya uuzwaji wa korosho ghafi katika msimu wa mwaka huu ambao unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi wa kumi.

Taratibu za ulipwaji wa korosho unamlazimu mkulima kuhakikisha anafungua akiba katika Taasisi za kifedha ili kuondokana na changamoto mbalimbali katika malipo kama vile kutapeliwa na wengine kuibiwa pindi wanapopokea pesa zao.

 

Kutokana na changamoto hiyo Kampuni ya simu za Mkononi ya  Tigo imefanya mchakato wakupitia majina ya wakulima wanaochukua pesa kupitia Tigopesa kwa lengo la kuweka usahihi wa majina yanayoandikishwa katika maghala ya kuhifadhi korosho.

 

 

John Tungaraza ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini anasema msimu wa mwaka jana 2017/2018 kulikuwa na changamoto ya tofauti ya jina la usajili katika Tigopesa na Jina lililoandikishwa mara baada ya kupeleka korosho Ghalani na hivyo kusababisha wakulima wengi kuchelewa kupata malipo yao kwa wakati.

 

 

“Tulichokifanya kwa msimu huu tumechukua wateja wetu wa Tigo na kufanya kitu kinaitwa Clean Up yaan Tumesafisha majina yote kwa ajili ya kuhakikisha Jina ambalo Limesajiliwa kwenye Usajili ya awali pamoja na Tigopesa zinaendana na tayari tumefanikiwa”Alisema Tungaraza.

 

Ameongeza kuwa  kikwazo kingine katika msimu uliopita ilikuwa kiasi cha ulipaji wa pesa kwa wakulima kutokana na mifumo wa mitandao wa sim ambao hauwezi kulipa zaidi ya Shilingi Million3 lakini katika msimu wa mwaka huu tayari swala hilo limefanyiwa kazi na sasa wataweza kulipa Shilingi Million kumi kupitia Tiogopesa.

 

“Tulipeleka maombi yetu Benki kuu ya Tanzania BOT yakuweza kulipa wakulima zaidi ya Million 10 kwa hiyo kwa msimu huu 2018/2019 wakulima wataweza kulipwa mpaka Million10 kwa hiyo tumejaribu kuondoa changamoto Tulizozipata katika msimu uliopita na sasa hivi kwa mkulima hahitajiki akipata ile pesa akaitoe pesa yote kwa wakala” aliongeza Tungaraza.

 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema Changamoto kubwa iliyokuwepo katika msimu uliopita  kwa wakulima wa korosho ni uelewa mdogo ambapo baadhi ya wananchii wamegoma kufungua akaunt katika taasisi za kifedha na badala yake kutumia akaunti ya mtu mwingine katika kupokea malipo yake na katika Tigopesa baadhi ya wananchii wamekuwa wakitoa maneno ya siri {Password} na hivyo kuibiwa pesa zake.

 

“Kwa Tigopesa wananchii wamekuwa wakitaja Maneneo ya siri kwa hiyo unakuta anakwenda sehem anataja namba ya siri na mtu anamuibia jambo ambali limeendelea kuleta malalamiko ya kuibiwa bilaya wao kujua”amesema Byakanwa.

 

Katika swala la kuchanganya majina ya vitambulisho na majina yaliyosajiliwa katika Tigopesa Byakanwa amewaomba Tigo kuhakikisha wanatoa elim kwa wakulima ili kuweza kufanya mfumo wa ulipaji wa pesa za korosho kuwa rahisi zaidi.

 

“Changamoto katika msimu ulipita ilikuwa ni kuchanganya majina ya kitambulisho na majina yaliyosjiliwa katika Line ya Tigopesa na tayari tumewaeleza tigo waongeze kasi katika kuhakikisha wanatoa elim ili kuondoa uelewa mdogo ili kurahisisha mfumo kuwa rafiki na kurahisisha malipo kwa Tigo Pesa”Byakanwa.

 

Abdallah Chiwewe ni mkulima wa korosho kutoka kijiji cha Mwena wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara anasema Pesa yake ya korosho kwa mwaka jana aliipata mapema  na kuanza kuipangia matumizi ya ujenzi wa nyumba yake.

 

“Nilikuwa shamba nikasikia mlio wa meseji kwenye sim nilipokwenda kutazama nikakuta malipo yangu ya kwanza ya korosho kupitia Tigopesa ndio nikaanza kutafuta fundi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madirisha ya nyumba yangu”amesema Chiwewe.

 

Naye Karim Mbunda ni mkulima wa korosho kutoka wilaya ya Newala Mkoani Mtwara anasema hakutegemea kupokea malipo yake ya korosho mapema zaidi akilinganisha na  miaka mingine ambapo malipo yamekuwa yakichelewa kuwafikia wakulima.

 

 

“mwaka jana malipo ya korosho yalichelewa na tulipokea kwa awam nyingi lakini kwa kutumia Tigopesa tulipokea malipo mapema na hatukutarajia”Mbunda.

 

Katika msimu wa mwaka 2017/2018 Jumla ya Vyama vya ushirika {Amcos} 44 katika Wilaya ya Masasi na Newala mkoani Mtwara Viliweza kulipa wakulima korosho kupitia Tigopesa.

 

Comments are closed.