The House of Favourite Newspapers

MO Dewji: Sikubali Kufanya Kazi na Mtu Anayehujumu Malengo

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameendelea kutoa kutoa kauli tata baada ya taarifa kusambaa mitandaoni zikidai kuwa wakati wowote atajiondoa katika klabu hiyo.

 

Taarifa hizo zilizoanza kusambaa juzi usiku katika mitandao ya kijamii, lakini mwenyewe amejitokeza na kuweka bayana kinachoendelea.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter pamoja na Instagram, Mo ameandika ujumbe mzito; “Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi – mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao.”

Ujumbe huu umepokelwa tofauti na mashabiki wa Simba ambao walikuwa wanahoji kuna tatizo gani ambalo limemkuta mwekezaji huyo kwa sasa.

Comments are closed.