The House of Favourite Newspapers

Mo Music afurahia kukosa meneja

0

mo musicStori: Boniphace Ngumije

MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amedai tangu aachane na meneja wake, Macdenis Mjata anafurahi kwa sababu mambo yake yanaenda vizuri tofauti na alivyokuwa chini yake.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Mo Music alisema kwa sasa mambo yake ya kimuziki anafanya kile anachotaka kwa wakati muafaka tofauti na awali alipokuwa akipangiwa kila kitu.

“Kazi zangu zinaenda kama kawaida na faida ni kubwa kuliko mwanzo, sina mpango wa kuwa na meneja kwa sasa, najisim-amia kwanza mwenyewe mpaka hapo nitakapoona kuna umuhimu wa kuwa na meneja ndiyo nitatafuta,” alisema Mo Music.

 

Leave A Reply