The House of Favourite Newspapers

Mobeto Atamba Kuoga Mamilioni

0

MWANAMAMA Hamisa Mobeto ni mrembo na staa ambaye kwa sasa anatingisha kutokana na kupata madili ya nguvu ya mamilioni anayolamba kila kukicha.

 

Ishu hiyo imemfanya Mobeto kutunisha mfuko wake wa pesa na kuonesha wazi milango yake ya baraka imefunguka huku mwenyewe akisema wakati wa Mungu ndiyo sahihi.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la mastaa nchini Tanzania baada ya kupata madili hao, Mobeto anasema kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo kwa sababu kila anapopita katika kipindi kigumu, Mungu huwa anamsimamia na kumuinua tena.

 

Mobeto anasema hayo yote yanatokana na Mungu kuamua kumvika utukufu mkubwa kuliko hata watu wanavyofikiria.

 

“Yaani kuna wakati mwingine naona Mungu ananifanya mimi kama mtoto wake wa mwisho, sijui nisemeje maana kuna milango ananifungulia, hata mimi nashindwa kuamini kama naweza kupata dili kama hilo maana ni madili mazuri mno kwa hiyo sina budi kumshukuru maana hata watu wakikuchafua kiasi gani, yeye anakusafisha,” anasema Mobeto ambaye ni baby mama wa watoto mawili.

 

Aidha, Mobeto au Misa anasema kuwa, atakuwa balozi bora kwa upande wa kuwahamasisha watu walipe kodi kama alivyopewa heshima hiyo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba na anahakikisha ataleta mabadiliko makubwa kwenye eneo hilo la uelimishaji wa watu kulipa kodi.

 

“Nafasi niliyopewa siwezi kuichezea hata kidogo kwa sababu kwangu ni heshima kubwa mno na ninahakikisha kuwa italeta mabadiliko makubwa na watu wengi watakuwa wanalipa kodi kwa hiyari,” anasema Mobeto.

 

Mbali na kuwa Balozi wa Kuelimisha Kulipa Kodi nchini Tanzania, pia ni balozi wa brandi nyingine nyingi zikiwemo za kinywaji maarufu duniani, nywele za kike, taulo za kike na matangazo ya kampuni mbalimbali ndani na nje ya Bongo.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

DIDA, KUMBILA la MOTO Walivyoshiriki CHAKULA Baada ya SHEREHE yao

Leave A Reply