The House of Favourite Newspapers

Mobeto: Nimechagua Kuishi Maisha Yangu na si Vinginevyo ndiyo Maana Sichuji

0
Hamisa Hassan Mobeto.

Hamisa Hassan Mobeto; ni mwanimitindo wa kimataifa na msanii wa muziki nchini Tanzania, ambaye anasema kuwa, katika maisha yake amechagua kuishi na siyo kukaa kama wengine wanavyoyachukulia maisha.

 

Mobeto anasema kuwa, kwa kufanya hivyo ndiyo maana hapati shida yoyote kutoka kwa waja wanaomzunguka kwenye maisha yake.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Mobeto anasema kuwa, anachopenda kwenye maisha yake ni kuishi bila stresi kabisa na ndiyo maana maisha yake yanasonga na madili yanazidi kuongeza kila kukicha kwa sababu moyoni ana furaha tele.

 

“Nimechagua kuishi maisha yangu mimi na si vinginevyo ndiyo maana kila kukicha sichuji na sichukii hata kidogo, maisha yangu ni mazuri kwa maana nina furaha moyoni mwangu na nina amani siku zote,” anasema Mobeto; mama wa watoto wawili mwenye madili kibao ya ubalozi.

Stori; Imelda Mtema, Dar

UCHAMBUZI wa BARAKA MPENJA: KOSA KOSA ya AZIZ KI, UBORA WA MAYELE – ”ZALAN TIMU DHAIFU”..

Leave A Reply