The House of Favourite Newspapers

Morogoro: Muuguzi Achomwa Kisu na Mgonjwa, Afariki

0

MTAWA muuguzi wa Kituo cha Kuhudumia Wagonjwa wa Ukoma cha Nazareth kilichopo Ifakara, Agatha Mbalalila (50), amefariki baada ya mmoja ya wagonjwa kudaiwa kumchoma kisu wakati akielekea kuwahudumia wagonjwa wengine kituoni hapo.

 

 

Katibu wa kituo hicho, Ladislaus Mloti, amesema marehemu alimpokea mtuhumiwa Februari 27, 2021 baada ya kufika kituoni na kujieleza kuwa ametoka katika matibabu ya ukoma Wilaya ya Bagamoyo.

 

 

Amesema mtuhumiwa hakuwa na matatizo ya akili wakati anapokelewa na waliamua kumlaza ili kumpatia matibabu ya vidonda alivyokuwa navyo mguuni ambapo baada ya kupona wangemruhusu arudi nyumbani.

Leave A Reply