The House of Favourite Newspapers

Moto California: 76 Wafariki, 1,300 Hawajuliani Walipo

Image result for North California fire

Jumla ya watu 76 wamethibitika kufa kutokana na moto wa msituni uliotokea California ya Kaskazini nchini Marekani ambapo maelfu ya watu wameachwa bila makazi na zaidi ya 1,300 hawajulikani walipo.

Moto huo ulioanza wiki iliyopita na wenye madhara zaidi kuikumba Marekani katika karne hii,  umeshuhudia mamia ya waokoaji wakipekua sehemu mbalimbali na kukuta mabaki ya miili ya watu, wakiwemo waliokuwa wakiishi katika mji wa Paradise uliotekelezwa.

Moto huo unaojuliakana kama ‘Camp Fire’ na ulioharibu nyumba zipatazo 10,000 na kuchoma ardhi ya kilomita za maraba 603, umethibitiwa kwa asilimia 55.

Rais wa Marekani, Donald Trump amelitembelea eneo hilo ambapo watu wapatato 1,300 hawajulikani walipo, ikiwa ni wiki moja baada ya kutokea kwa moto huo.

Mji wa Paradise wenye wakazi 26,000, pembeni yake pamejengwa kambi ya watu 50,000 waliokimbia kutoka sehemu mbalimbali kukwepa moto huo.

Related image

 

Comments are closed.