The House of Favourite Newspapers

Mourinho Ampa Makavu Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza Kuhusu Abraham

0
Mshambuliaji wa AS Roma, Tammy Abraham

KOCHA wa klabu ya AS Roma ya nchini Italia Mreno Jose Mourinho ameibuka na kumpa makavu kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate kutokana na uamuzi wake wa kumuacha mshambuliaji Tammy Abraham katika kikosi cha Uingereza kinachoenda Kombe la Dunia nchini Qatar.

 

Mourinho amehusisha kitendo hicho na suala la ubaguzi wa rangi kutokana na kuwa Abraham ana rangi nyeusi na ana asili ya Nigeria.

Jose Mourinho, Kocha wa Klabu ya AS Roma ya Italia

“Gareth Southgate amesema Tammy Abraham amekuwa na k,iwango kibovu cha kufunga katika wakati mbaya, ni utetezi wa kitoto. Analazimika kuibuka na kusema wazi kuwa hapendezwi za rangi ya Tammy kwasababu Kelvin Philips amecheza dakika 56 tu na amechaguliwa. Mimi kama Tammy ningeenda FIFA na kufungua jarada la kulalamika kuwa nimeharibiwa maendeleo ya soka langu katika ngazi ya timu ya taifa kwahiyo nipewe kibali cha Kwenda kuwakilisha timu ya taifa ya Nigeria. Huo ndiyo ushauri wangu. Nichukie lakini ndiyo umeshaamua.” amesema Mourinho.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate

Baadhi ya nyota ambao wamejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza na kuibua maswali mengi ni pamoja na mlinzi wa kati wa klabu ya Manchester United Harry Maguire ambaye amejumuishwa mbele ya Fikayo Tomori licha ya kuwa Maguire amekuwa akikaa benchi kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha Manchester United.

Leave A Reply