The House of Favourite Newspapers

Mpemba Kinara wa Meno ya Tembo Aliyetajwa na Rais Magufuli Apandishwa Kortini

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-8 DAR ES SALAAM: MTUHUMIWA wa makosa ya kukamatwa na nyara za serikali, Yusuf Ali Yusuf maarufu kama Shehe Mpemba (35)  ambaye alitajwa na Rais John Magufuli kuwa ndiye kinara wa biashara ya meno ya tembo, leo amesomewa mashitaka manne yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba.

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-9Mtuhumiwa wa makosa ya kukamatwa na nyara za serikali, Yusuf Ali Yusuf ‘Shehe Mpemba’ (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake mahakamani.

Mpemba na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kula njama za kufanya uhalifu na kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria.

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-6…Watuhumiwa wakipandishwa mahakamani.

Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Paul Kadushi,  alisema kwa nyakati tofauti kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016, jijini Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara, watuhumiwa hao walitenda makosa hayo.

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-10

Mtuhumiwa huyo na wenzake Charles Mrutu (37), Benedict Kungwa (40), Jumanne Chima (30), Ahmed Nyagongo (33) na Pius Kulagwa (46)  hawakutakiwa kujibu chochote na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba Mosi, mwaka huu itakapotajwa tena huku watuhumiwa hao wakirudishwa rumande.

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-7…Watuhumiwa wakiwa mahakamani.

Mwezi Oktoba mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini hapa, alimtaja Mpemba kwamba amekuwa akisikia habari zake kwenye taarifa za kuhusika na biashara hiyo haramu na kuwapongeza waliofanikisha kukamatwa kwake.

IFUATAYO NI HATI RASMI YA MASHITAKA YA WATUHUMIWA:

kisutu1 kisutu2 kisutu3 kisutu4 kisutu5

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.