The House of Favourite Newspapers

MPENZI WA MBASHA ACHUMBIWA

ALIYEWAHI kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Injili, Emmanuel Mbasha ambaye pia ni mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa ‘Jack’ amechumbiwa na ndoa yake inatarajiwa kufanyiwa hivi karibuni.

Chanzo makini kililiambia Za Motomoto News kuwa, Jack amevishwa pete ya uchumba na mchungaji mmoja wa kilokole ambaye kanisa lake liko Moshi mkoani Kilimanjaro licha ya kwamba mwanadada huyo amekuwa akifanya siri.

Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Jack ambapo alikiri kuchumbiwa na mchungaji ambaye ana kanisa huko Moshi lakini hayupo tayari kutaja jina lake wala kanisa lake kwa kuwa siyo maadili ya kanisa lao. “Ni kweli nimechumbiwa na nitaolewa hivi karibuni, jina la mchumba wangu siwezi kuliweka wazi maana ni mchungaji hivyo kimaadili hairuhusiwi,” alisema Jack.

Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Comments are closed.