The House of Favourite Newspapers

MPOTO ATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA DAR

Mwanamuziki  wa Muziki wa Asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la ‘Mjomba’ akiwagawia juzuu wanafunzi wa madrasa.

Mpoto akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa madrasa  ya Tidaiya iliyopoTandale.

…Akikabidhi misahaafu kwa mmiliki wa madrasa ya  Tidaiya iliyopo Tandale, Nassoro Omary (kulia).
Mrisho Mpoto akitoa mikeka kwa ajili ya wanafunzi wa madrasa wa kituo cha Tandale.
Mwanamuziki  wa Muziki wa Asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la ‘Mjomba’ akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa baada ya kufika kituoni hapo.
...Mpoto akiteta jambo na watoto yatima wa Mwandaliwa.
Mkurugenzi wa Kituo  cha Mwandaliwa,  Halima Ramadhani (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zawadi alizozipokea kutoka kwa Mpoto.
…Akila chakula na watoto wa kituo cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni.
…Akikabidhi misahafu  kwa watoto hao.
Akikabidhi  juzuu kwa watoto watoto wanaolelewa katika kituo cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 

MWANAMUZIKI wa Muziki wa Asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la ‘Mjomba’, ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro, leo ametoa msaada wa mikeka, misahaafu na juzuu kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopoTandale.

 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.

 

Mpoto alisema: “Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.”

 

Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.

 

Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.

 

Comments are closed.